Featured Kitaifa

RC KAFULILA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

Written by mzalendoeditor

NA Mwandishi Wetu-SIMIYU

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila, ametoa siku 14 kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani humo, kuhakikisha wanakamilisha uandikishaji wa anuani za makazi.

Zoezi la Uandikishaji wa Anuani za Makazi katika Mkoa huo limekua likienda kwa kusuasua hali iliyofanya Mkuu huyo wa Mkoa kuingilia kati ili kuongeza kasi katika utekelezaji wake.

Maagizo hayo yanawahusu wakuu wa Wilaya na Wakurugezni wa Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu na kwa mujibu wa Mku huyo wa Mkoa ni kwamba utekelezaji wake unatakiwa kuanza mara moja

About the author

mzalendoeditor