KOCHA wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi amesema klabu yake ya Orlando Pirates haikustahili kufungwa katika mchezo huo kutokana na kwamba Penati haikuwa sahihi kwa simba kupewa.
Mandla ameyasema hayo mara baada ya mchezo kumalizika, ametumia muda mwingi kuwalaumu waamuzi pamoja na kuhoji matumizi ya VAR kwani amedai kabla ya simba kupewa mkwaju wa penati nao pia walistahili kupata mkwaju wa penati.
Mchezo kati ya Simba SC na Orlando Pirates ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililowekwa kimiani na mlinzi wa kulia wa Klabu hiyo Shomari Kapombe.