MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema uwanja wa ndege wa Singida ni muhimu kutokana na mkoa huo kuwa karibu na Makao Makuu
ya Nchi Dodoma na kutokana na sababu za kiusalama.
Mtaturu amesema hayo April 14,2022,Bungeni Jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza.
“Marais wote wawili Hayati John Magufuli na Rais Samia Suluhu Hassan walisema katika viwanja 11 kiwanja cha Singida kitajengwa, sasa naomba kujua lini serikali itatenga fedha kujenga uwanja ule ambao upo karibu na Makao Mkuu ya Nchi,”ameuliza.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya amekiri viongozi hao kuahidi ujenzi wa uwanja huo na kusema wizara ina mpango wa kufanya tathmini ya uwanja huo ili uanze kujengwa.