Featured Kitaifa

AVUNJWA MIGUU NA MIKONO BAADA YA KUFUMANIWA NJOMBE

Written by mzalendoeditor

Njombe

Kijana anayefahamika kwa jina Benard Mkolwe mkazi wa kata ya Madilu,wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,amepigwa na kuvunjwa mikono na miguu baada ya kukutwa na msichana Sara Mgohole anayedaiwa kukutana naye nyumbani kwao kwa lengo la tendo la ndoa ikiwa ni siku ya kwanza tangu waanze mahusiano wiki mbili zilizopita.

Kijana huyo amekili kuwa na mahusiano na msichana huyo na kudai kuwa mahusiano yao yalikuwa yakuwasiliana kwa simu pekee na yana muda wa wiki mbili toka wayaanzishe hivyo siku ya tukio hilo ilikuwa ni siku yao ya kwanza kukutana kwa lengo la kufanya tendo la ndoa.

“Waliofanya tukio ni baba zake wadogo wa yule binti yule binti ni kama wiki mbili tuko kwenye mahusiano lakini sijawahi kufanya kitu chochote kile tulikuwa ni marafiki wa kuchati na ile siku alivoniita nahisi ndio ilikuwa siku ya kuelekea kwenye tendo lakini sikufanya kitu chochote”alisema Benard Mkolwe

Kijana huyo anafanyiwa matibabu katika hospitali ya St. Jon’s huku Daktari wa zamu wa hospitali hiyo Zainabu Said akieleza kuwa kijana huyo ameumizwa na sasa anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo sambamba na kupinga vikali vitendo vya wananchi kujichulia sheria mkononi.

“Labda kuna visa vya awali,huu ni ukatili wa kijinsia unaotokana na binti kusuka mpango kumuonea huyu kijana,yeye amekubali kuchati halafu wanakuja kumpiga na kama alikuwa hana uhitaji wa kukutana na huyu kijana angemkatalia toka mwanzo”alisema Tsere

CHANZO:MUUNGWANO BLOG

About the author

mzalendoeditor