Featured Michezo

WALIMU WASHAURIWA KUWA NA RATIBA YA MICHEZO SHULENI NA SIO KUSUBIRI UMISSETA NA UMITASHUMTA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Michezo Ofisi ya Rais TAMISEMI Leonard Thadeo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa walimu wa michezo wa shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Dodoma leo April 12,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma Justine Machela akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa walimu wa michezo wa shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Dodoma leo April 12,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa walimu wa michezo wa shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Dodoma leo April 12,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Michezo Ofisi ya Rais TAMISEMI Leonard Thadeo  akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mafunzo kwa walimu wa michezo wa shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Dodoma leo April 12,2022 jijini Dodoma.

……………………………………………..

Na Bolgas Odilo, Dodoma.

 

WALIMU wa michezo Mkoa wa Dodoma washauriwa kuwa na ratiba ya michezo kwa wanafunzi shuleni mara kwa mara na si kusubiri raiba za UMISSETA na UMITASHUMTA kwani kwa kufanya hivyo kutawaondelea maradhi ya hapa na pale.

Kauli hiyo imetolewa leo 12 Aprili 2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Michezo Ofisi ya Rais TAMISEMI Leonard Thadeo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya walimu wa michezo Mkoa wa Dodoma.

“Msisubiri ratiba za UMISSETA na UMITASHUMTA, mnataka watoto wenu wafanye vizuri na maisha mazuri katika michezo basi wakati wote muwajengee utaratibu wa kushiriki michezo wakiwa shuleni kwa sababu nafasi yao kubwa ni kuwa shuleni.

“Kufikia Desemba 2021 tulikuwa na watoto 26 wanaochezea Ligi daraja la kwanza, hawa watoto wametokana na michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ukiacha ile ya wanaochaguliwa kujiunga na Timu ya Taifa ya vijana kuanzia miaka 17,” alisema Thadeo.

Aidha Thadeo aliwataka walimu kuzingatia yote watakayoelekezwa kwenye mafunzo hayo yatakayotolewa ili wakawe mabalozi wazuri warudipo kwenye Halmashauri zao.

“Dodoma hatutaamka kama tutakuwa hapa kwaajili ya mafunzo halafu tukitoka hapa tusiende kuyafanyia kazi yale tuliyojifunza, tutakua watu wa kufungwa tu kwenye UMITASHUMTA hadi UMISSETA.

“Matarajio yetu ni kwamba, mkitoka hapa mafunzo mliyoyapata mtaenda kuwapelekea wengine ili iweze kusambaa katika shule zote na kwa kufanya hivyo tunaweza kufika mbali.

“Kufikia Desemba 2021 tulikuwa na watoto 26 wanaochezea Ligi daraja la kwanza, hawa watoto wametokana na michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ukiacha ile ya wanaochaguliwa kujiunga na Timu ya Taifa ya vijana kuanzia miaka 17.

“Tukafanye kazi, mkoa umeona kwamba ninyi mnaweza kusaidia kuutangaza mkoa kwa kufanya kazi,” alisisitiza Thadeo.

Pia Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Justine Machela alisema kuwa mpango wa Mkoa wa Dodoma ni kuona kiwango cha michezo kinakua na kuwapa fursa wanafunzi kuonesha ujuzi wao na watambue kuwa michezo ni ajira.

Kwa upande wao walimu waliohudhuria kwenye mafunzo hayo walionesha utayari na kuunga mkono agizo la Mkurugenzi wa Michezo Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuhakikisha wanaleta mabadiliko kwenye nyanja hiyo.

About the author

mzalendoeditor