Featured Kitaifa

RIPOTI YA CAG YAIBUA MADUDU KWENYE MFUMO WA BIMA YA AFYA,

Written by mzalendoeditor

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 12,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu  uwasilishaji wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni,2021.  

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 12,2022 jijini Dodoma mara baada ya kutoa taarifa kuhusu  uwasilishaji wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni,2021.  

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) Mhe.Grace Tendega,akizungumza mara baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere,kutoa taarifa kuhusu  uwasilishaji wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni,2021 leo April 12,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere,(hayupo pichani) leo April 12,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu  uwasilishaji wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni,2021. 

…………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere amesema kunamapungufu ya uthibiti kwenye Mfumo wa madai wa mfuko wa Bima ya Afya ambapo amebaini madai 56 yanayoonyesha wanaume walipata huduma ya upasuaji (C/S) au huduma za kawaida za kujifungua wakati huduma hizo hutolewa kwa wanawake tu.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 12,2022 jijini Dodoma  wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uwasilishaji wa Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni ,2021.

Amesema pia ukaguzi wake umebaini wanachama 444 waliopata huduma za kuchunguzwa picha kamili ya damu (Full blood picture) zaidi ya mara moja kwa siku moja (Hadi mara 30) kwenye Kituo kimoja cha .

Aidha amesema kuwapo kwa malipo ya madai yaliorudiwa Pamoja na madai yanayoonesha mwanachama wa NHIF walipokea Miwani ya kusomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja kwa Mwaka.

“Udhaifu huu imesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika Mfumo wa madai iliyosababisha hasara ya Shilingi Millioni 14.41 kwa mfuko,” amesema Mdhibiti huyo.

Na kuongeza Kusema “Napendekeza kwamba mfuko wa Bima ya Afya : (a) Kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa watoa huduma za Afya husika ; na (b) kuboresha Mfumo wa madai wa CMIS ili kuhakikisha kuwa unasaidia Maafisa wanaohusika kuangalia uhalili wa madai yalio wasilishwa .

KWA UPANDE WA MAFUTA

Hata hivyo amebaini Mafuta kuingia yalioingia nchini bila kuainishwa Kama Ni yamatumizi ya ndani au kusafirishwa nchi jirani yenye ushuru wa forodha Shilingi Bilioni 2.89.

Amesema alibaini Miamala 17 yenye jumla ya Lita Milioni 31.12 zenye makadirio ya ushuru wa forodha Shilingi Bilioni 2.89 ambayo hayakuainishwa Kama ni kwamatumizi ya ndani au yakusafirishwa kwenda nchi jirani .

“Hii inahashiria kwamba Mafuta hayo yalitumika nchini na yalipaswa kutozwa ushuru Shilingi wa forodha Shilingi Bilioni 2.89 ,”amesema Kichere .

Nakuongeza”Ninapendekeza kwamba Serikali iimarishe mifumo ya udhibiti na usimamizi wa mafuta yanayoingia nchini ili kuzuia matumizi ya Mafuta hayo nchini bila Kodi stahiki kulipwa,”amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

About the author

mzalendoeditor