Featured Kitaifa

MANARA AZIDI KUMVURUGA MAKONDA,NANI AKUUE WEWE, ULITESA WATU…HEBU KWENDA ZAKO”

Written by mzalendoeditor

Screenshot_20220412-005922_InShot

Msemaji wa Timu ya mpira wa miguu ya Klabu ya Yanga, Haji Manara amemvaa Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya  makonda kudai kuwa, kuna mkakati unaoratibiwa na makundi matano kwa ajili ya kuangamiza maisha yake. 
Baada ya kuandika maneno hayo Msemaji wa Timu ya mpira wa miguu ya Klabu ya Yanga, Haji Manara amemjibu Makonda kupitia post yake katika comment kuwa;


Anaitwa Mungu,,mkweli na kwa sasa hachelewi kujibu,,leo unatafuta sympathy huku ukijua nn ulwafanyia watu?
Dhulma,dharau,kejeli,matusi na hata kuwaona Viongozi wenzio hawana maana,,ukawabambizia kesi za unga watu,,ukanyang’anya watu magari yao,Sisahau siku uliyokataa kukaa jukwaani Pale Kwa Mkapa na kukaa ktk benchi kama Kocha kisa hutaki kusalimiana na mkubwa wako eti kisa hakupendi,,Umesahau hata Mtoto wa mkubwa ukasema anauza unga na kutaka kumchafua kisa ulipata Cheo?

Acha kumsingizia Mungu,,waombe msamaha watanzania kwa dhulma zako,,na usitegemee Serikali ikuonee huruma,,inajua everything about you,,kina Sudi ukawasweka ndani bila sababu,,mm ndio nilikuwa mnyonge wako,,hebu kwenda zako,,akuue Nani ww ? Utajiua kwa stress zako mwenyew,,cheo huna nenda kolomije kavue Sangara

IMG_20220412_002139
IMG_20220412_002415
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa, kuna mkakati unaoratibiwa na makundi matano kwa ajili ya kuangamiza maisha yake.
Makonda ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiyataja makundi hayo na kujiuliza mambo mawili.
Kutoka Page ya Instagram ya Paul Makonda:
“Nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na Makundi 5 kuangamiza maisha yangu.
 
 
1) WAUZA MADAWA YA KULEVYA
2)WANUFAIKA NA MADAWA YA KULEVYA
3) MASHOGA
4)WANAOKESHA USIKU KUCHA KUTAFUTA KULIPA KISASI KWA WASAIDIZI WA DR MAGUFULI.
5) WALIOWAHI KUWA SEHEMU YA ……. Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida ya familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi.
 
 
Mambo mawili najiuliza
1)PAMOJA NA KAZI ZOTE NZURI NILIZOZIFANYA KWA CHAMA CHANGU,SERIKALI YANGU NA WANANCHI WA DAR HAYA NDIYO MALIPO YAKE?
2)Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndiyo malipo yake ?
 
 
MTU aliejemga hospital , aliejenga ofc cha CCM, Magari ya police ?‍♀️, ofc za Walimu, vituo vya police, shule za secondary mpaka na msingi, kutibu wagonjwa mpaka Meli kuja Tanzania,kuhudumia Makundi mbali mbali mpaka kuiunganisha Serikali na Viongozi wa Dini. leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa.
 
 
Pamoja na kwamba lipo kundi kwenye mitandao linalolipwa ili kuwaanda watanzania pale watakapo nikamata ionekane ni sawa. Hakika ipo siku Walemavu, yatima, wajane na waliotamani watoto WAO wasife kwa MADAWA ya KULEVYA SAUTI ZAO ZITASIKIKA.
 
 
#Ukiona maji yametulia jua kina nikilefu” Makonda

About the author

mzalendoeditor