Featured Kitaifa

CHONGOLO AMTEMBELEA ALI MASOUD KIPANYA NA KUJIONEA UBUNIFU WA GARI

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Ali Masoud ‘Kipanya’ (kulia) mara baada ya kutembelea karakana yake ya Kaypee Motors iliyopo eneo la Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) Vingunguti, jijini Dar Es Salaam, kujionea gari inayotumia nguvu za umeme iliyobuniwa na Kipanya, ikiwa gari ya kwanza ya aina hiyo kubuniwa na Mtanzania.
 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akisaini kitabu cha wageni katika Karakana ya Kaypee Motors ya Ali Masoud ‘Kipanya’ iliyopo katika eneo la Shirika la Viwanda Vidogovidogo (SIDO) Vingunguti, jijini Dar Es Salaam ambapo alifika hapo kutembelea na kujionea gari inayotumia nguvu za umeme, iliyobuniwa na Kipanya, ikiwa gari ya kwanza ya aina hiyo kubuniwa na Mtanzania.

About the author

mzalendoeditor