Featured Michezo

YANGA YATANGULIA NUSU FAINALI YA ASFC YAISUBIRI SIMBA

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna

YANGA imetinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) baada ya kuitoa Geita Gold kwa  mabao 7-6 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Geita walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 86 likifungwa na Offen Chikola na Shaban Djuma aliisawazishia Yanga dakika ya 90 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na ikapelekea kwenda kwenye Mkwaju wa Penalti.

Shujaa wa Yanga ni  mlango wa Yanga Raia wa Mali, Djigui Diarra ‘Screen Protector’ alipangua Penalti ya mwisho ambayo ilipigwa na Juma Mahadhi huku pia Diarra akikosa Penalti ya sita baada ya kupiga nje.

Kwa Matokeo Yanga wametinga Nusu Fainali na watakutana mshindi kati ya Simba au Pamba kutoka jijini Mwanza mchezo utakaopigwa kati ya Arusha au Mwanza.

About the author

mzalendoeditor