Featured Kitaifa

SAGINI ATAKA WAKURUGENZI WAMILIKI WA MAKAMPUNI BINAFSI YA ULINZI TANZANIA KUSHIRIKIANA.

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwasili katika Ukumbi wa Rukane katika Hoteli ya New Dodoma Hotel jijini Dodoma, leo Aprili 8, 2022 katika Kongamano la Wakurugenzi wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza katika Kongamano la Wakurugenzi Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi Tanzania Bara na Zanzibar kilichofanyika leo April 8,2022  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi Tanzania Bara na Zanzibar kilichofanyika leo April 8,2022 ,jijini Dodoma.

………………………………………………

Na Mwandishi wa MoHA,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jummanne Sagini, amewataka Wakurugenzi Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi, Tanzania kuwa na ushirikiano baina yao ili kuleta hoja zao kwa umoja Serikalini, sambamba na kuwataka kufanya kazi zao kwa weledi zaidi.

Naibu Waziri Sagini ameyasema hayo leo wakati wa Kongamano la Wakurugenzi Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi lililofanyika katika ukumbi wa New Dodoma hoteli, jijini Dodoma.

“Maadamu mpo kwenye kada moja kumbukeni kuwa umoja ni nguvu, shirikianeni katika kazi yenu ili muendelee kulinda usalama wa raia na mali zao nchini” alisema

Akizungumza na Wakurugenzi Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi, Naibu Waziri amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani wamekuwa na mchango mkubwa sana wa kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa Nchi yenye utulivu na amani.

“Serikali inatambua mchango wa Jeshi la Polisi pamoja na Makampuni Binafsi ya Ulinzi katika kuhakikisha hali ya usalama na utulivu inaendelea kushamiri hapa nchini Tanzania. Hali hii imewezesha shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali unaendelea bila hofu yeyote”

Aidha, amewataka Wakurugenzi Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi kuanzisha kanzi data kwenye makampuni zao ili kuweza kutunza taarifa za wafanyakazi pamoja na kuratibu kazi zao za ulinzi.

Naibu Waziri Sagini ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Makampuni Binafsi ya Ulinzi na kuwata kuendelea kuratibu mafunzo ya ulinzi kwa watumishi wa makampuni hayo.

Hata hivyo, Naibu Waziri Sagini amewapongeza Maafisa wa Jeshi la Polisi wastaafu waliochukua jukumu la kuanzisha Makampuni Binafsi ya Ulinzi, halib inayowafanya waendelee kutekeleza jukumu la kuleta amani na utulivu Nchini.

About the author

mzalendoeditor