Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AONGOZA WANANCHI WA ZANZIBAR KATIKA DUA YA KUMUOMBEA RAIS WA KWANZA NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI HAYATI SHEIKH.ABEID AMANI KARUME AFISI KUU YA CCM ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Samia Suluhu Hassan wakielekea katika kaburi la Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh.Abeid Amani Karume, kwa ajili ya kumuombea dua na kuweka mashada ya maua katika kaburi, baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhja Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kulia kwa Rais) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Amani Abeid Karume na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango, wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, wakimuombea Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh.Abeid Amani Karume, wakiwa katika kaburi baada ya kumalizika kwa Dua na kisomo cha kumuombea marehemu kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh.Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo na dua ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar 

Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor