Kitaifa

ZAIDI YA WANAWAKE 500 KUPATA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI WATOTO

Written by mzalendoeditor
Waliopo pichani ni watoto mapacha waliopatikana baada ya huduma hiyo ya upandikizaji watoto wakiwa wamebebwa na madaktari ,aliyesimama kushoto mwenye kofia nyekundu ni Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi ,Dokta Nicholaus Mazuguni
Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi ,Dokta Nicholaus Mazuguni akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma hiyo inayotolewa hicho.(Happy Lazaro)
………………………………………….
Happy Lazaro, Arusha.
Arusha.Changamoto ya uzazi iliyokuwa ikisumbua familia nyingi na kufuata huduma hiyo nje ya nchi,hivi Sasa imepata mwarobaini baada ya kituo cha kutolea huduma ya uzazi na upandikizaji mimba cha  Avinta Care Medical kilichopo mjini hapa kwa mara ya kwanza kuja na huduma ya upandikizaji watoto Jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika kituo hicho ,Dokta Nicholaus Mazuguni amesema kuwa, walianza kutoa huduma hiyo ya upandikizaji watoto tangu mwaka 2017 wakishirikiana na wataalamu kutokana hospitali ya Muhimbili.
Dokta Mazuguni amesema kuwa,tangu wameanza kutoa huduma hiyo idadi ya watu wanaofika kituoni hapo kupata huduma kwa wiki ni zaidi ya mia moja ambapo wengi wao wameonekana kuwa na matatizo ya uzazi na kuweza kuanzishwa matibabu kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
“Tangu tulipoanza  kutoa huduma hii mwaka 2017 tumeshapandikiza wanawake zaidi ya 500 na kufanikiwa kupata watoto zaidi ya 250 waliopatikana  kutokana na huduma hiyo , na mwitikio ni mkubwa sana kwani watu wengi walikuwa wanatumia gharama ya kwenda nje ya nchi ila kwa Sasa hivi wanapata huduma hiyo hapa hapa bila shida yoyote.”amesema Dokta Mazuguni.
Ameongeza kuwa,wamekuwa wakipandikiza watoto mapacha hadi watatu kulingana na uhitaji wa mgonjwa kwani wengi wao unakuta wamekaa muda mrefu bila kupata mtoto ,hivyo wanakuwa na uhitaji mkubwa zaidi.
“Mara ya mwisho tumempandikiza mwanamke mwenye miaka 50 watoto mapacha na amefanikiwa kupata watoto wake vizuri Sana bila shida yoyote na kweli wengi wao huwa wanafurahi Sana kwani wameteseka na kukutana na changamoto nyingi katika kutafuta watoto na gharama zetu za utoaji wa huduma hiyo ni kuanzia milioni 7 na kuendelea kulingana na umri wa mgonjwa”amesema.
Hata hivyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Samia Suluhu kwa jitihada kubwa alizoonyesha kwenye maswala ya Afya ya uzazi kwa akinamama kwani ni hatua kubwa sana kutokana na huduma hizoe kupatikana popote kwa wanaohitaji. 
Ameongeza kuwa, changamoto iliyopo katika  familia kubwa ni kuwatupia lawama wanawake kuwa ndio wenye matatizo hayo ,jambo ambalo amesema kuwa,wanaume pia wanakumbana na changamoto hiyo ya uzazi hivyo ni vizuri wakafika wote kwa pamoja kituoni hapo kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu .
Kwa upande wake Daktari wa akinamama kutokana hospitali ya Muhimbili ,Dokta Hildegarda Aloyce amesema kuwa,wamekuwa wakishirikiana na kituo hicho cha Avinta katika kutatua changamoto za uzazi kwani tatizo hilo bado ni kubwa katika jamii  ambapo kati ya wagonjwa 10  ambao wamekuwa wakipokelewa wagonjwa 4 hadi 6 wana  tatizo la uzazi .
Mganga Mkuu  wa mkoa ,Dokta Sylvia Mamkwe amepongeza juhudi hizo zilizofanywa na kituo hicho kwa kushirikiana na hospitali nyingine,na Kama serikali wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha huduma hiyo ili kuwahudumia wagonjwa wengi zaidi.
Mmoja wa wanufaika kutokaa wilayani Simanjiro, Martha Sangwa amesema kuwa, amefurahishwa Sana kwa huduma hiyo iliyomfanikisha kupata watoto mapacha kwani ameteseka kwa miaka 16 bila msaada wowote,hivyo uwepo wa kituo hicho ni faraja kubwa  Sana kwao na kuwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo.

About the author

mzalendoeditor