Featured Kitaifa

SERIKALI KUTANGAZA AJIRA MPYA 32,000

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Rais Samia Hassan amekubali kutoa ajira za watumishi wa Umma wapya zaidi ya 32,000.

Mhagama amesema hayo leo Aprili 6,2022 Bungeni Dodoma wakati wa Kipindi cha Bunge cha Maswali na Majibu.

Amesema kuwa wiki ijayo wizara yake itatangaza rasmi ajira hizo 32,000 ambazo kipaumbele ni kwenye sekta ya Elimu na afya.

About the author

mzalendoeditor