Manchester City imeanza vyema kampeni ya kutafuta ubingwa baada ya kuichapa bao 1-0 ya Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Shujaa wa Man City ni kiungo mshambuliaji Kevin De Bruyne dakika ya 70 aliifungia bao muhimu Manchester City.