Featured Kitaifa

IGP SIRRO AFUNGUA KITUO CHA POLISI CHA KISASA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka watendaji wa Jeshi hilo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi kwa kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu na wahalifu wanazokutana nazo.

IGP Sirro amesema hayo wakati akifungua kituo cha Polisi cha kisasa kilichopo uwanja wa ndege wa Dodoma mkoani Dodoma ambapo ambao ujenzi wa Kituo hicho cha Polisi na nyumba ya Mkuu wa Kituo cha Polisi umegharimu kiasi cha milioni 115 hadi kukamilika kwake.

Kwenye ufunguzi huo IGP Sirro pia amesema kuwa, ni vyema viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kuwa macho na kuongeza umakini hasa katika kubaini wahalifu, waingizaji wa dawa za kulevya na wamakosa mengine kutokana na uwanja huo kutumiwa na watu mbalimbali kwa shughuli za usafiri wa anga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweli akimuwakilisha Mkuu wa mkoa huo Mhe, Antony Mtaka amesema kuwa, wilaya imeendelea kuhamasisha ufungaji wa kamera za usalama kwa ajili ya kuimarisha udhibiti wa uingizaji wa dawa za kulevya sambamba na uhalifu mwingine.

About the author

mzalendoeditor