Featured Kitaifa

WAZIRI MABULA ATOA TAHADHARI KWA WANAOVAMIA MAENEO

Written by mzalendoeditor

p class=”MsoNormal”>

WAZIRI wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya
Mawaziri sita wa kisekta wakiongozwa na Waziri huyo pamoja na viongozi wa mkoa
wa Tanga kulia  ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
     

 

WAZIRI wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makaz Dkt Angelina Mabula akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya
Mawaziri sita wa kisekta wakiongozwa na Waziri huyo pamoja na viongozi wa mkoa
wa Tanga
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Allan Kijazi akizungumza wakati wa kikao hicho
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa kikao hicho

MBUNGE wa JImbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akifuatilia kikao hicho

 

 NA OSCAR
ASSENGA, TANGA

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Dkt Angelina Mabula amewatahadharisha wananchi wenye tabia za kuvamia maeneo na
kutegemea kwamba serikali itaridhia waendelee kuwepo jambo hilo halitajirudia tena.

Dkt Mabula
aliyasema hayo leo mjini Tanga mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati ya
Mawaziri sita wa kisekta wakiongozwa na Waziri huyo pamoja na viongozi wa mkoa
wa Tanga.

Alisema ziara
yao ni ya kwenda mkoa kwa mkoa kushughulia suala migogoro ya ardhi kwenye
Vijiji 975 ambavyo baraza la mawaziri limeridhia viende kufanyiwa marekebisho
au vingine kuondoshwa na vingine vifanyiwe mpango wa matumizi kutokana na
maamuzi yatakayotoka

Alisema wakishafanya
hivyo hawatarajii kuona kutakuwa na maeneo ya urasimishaji au kuridhia kumegwa
maeneo watahitaji kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake kwa kutii sheria bila
shurui maana hawawezi kuwa na mazoezi kama hayo kila mwaka

Alisema
kwamba wameongea na viongozi wa mkoa wa Tanga hasa maadhimio waliyokubalina na
baraza la mawaziri na Rais ameridhia waanze kupita kwenye mikoa ili waweze
kutoa taarifa hizo ili mikoa wahusika na utekelezaji wake yaliyoamuliwa na
serikali.

Waziri huyo
alisema kwa mkoa wa Tanga kuna vijiji 18 kati ya vijiji 975 ambapo kati ya vijiji
hivyo vijiji 14 kuna marekebisho kadhaa yatafanyika ,vijiji 4 kulingana na hali
halisi wanaiona mustakabali wa nchi kama wataviachi viendelee kuwepo athari
zake zitakuwa ni kubwa zaidi wanakwenda kufanya tathimini kuweza kujua hatma ya
vijiji hivyo baada ya wao kuondoka wataacha timu mkoani Tanga.

Alisema timu
hiyo itapita kwenye maeneo hayo wakifanya tathimini na mwisho wa siku
watapeleka ushauri kwa serikali hatua za kuchukua lakini pamoja na tathimini
mkoa kama mkoa watajipanga kwa ajili ya utekelezaji.

“Leo ilikuwa
ni kuwapa maamuzi ya baraza la mawaziri ambayo yana baraka za Rais Samia Suluhu
kwa hiyo suala la utekelezaji wanaanzia wapo ni jukumu la mkoa na timu yake,ushirikishwaji
katika suala zima la utekelezaji maamuzi hayo ili isitokee mtu akalalamikia
kuonea au kufanyaje jukumu lao kama serikali ni kuhakikisha wanatoa elimu ili
masuala hayo yasijirudie”Alisema

Alisema kwa
sababu wamekuwa na operesheni mbalimnbali mwisho wa siku usimamizi wake unakuwa
sio mzuri matokeo yake yanajirudia kipindi hiki chini ya Rais Samia Suluhu angependa
kuona mambo hayo yanajirudia na ndio maana kwenye wizara ya ardhi ameridhia
kutoa fedha nyingi ili waweze kumalizikana na migogoro ya watumiaji ardhi.

Waziri huyo
alisema hivyo wanalolifanya ni mendelezo kuona kila mmoja awajibike ndio maana
alisisitiza Mkuu wa mkoa ,Wilaya,Maafisa Tarafa na watendaji chini kila mmoja
akisisimie jukumu lake suala kama hilo halitaweza kujirudia tena,

“Lakini nitoe
rai kwa wananchi watakaokuwa wametengewa maeneo na  kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi
hatutarajii kuona mnaingi maeneo ya hifadhi yaliyozuiliwa ,mnaingiakwenye
maeneo ya vyanzo vya maji,maeneo ya taasisi mbalimbali ambazo wamekuwa
wakivamia maana hayo ndio yametufikisha hapa tulipo”Alisema Waziri Dkt Mabula

Hata hivyo
alisema kila mmoja watumishi wa serikali na watendaji wanayo nafasi yao katika
kufanya usimamizi mambo hayo yasijirudii ikiwemo wananchi watii sheria bila
shurti.

“Lakini
niwaambie kwamba kwamba kwa wale ambao wanavamia maeneo na kutegemea serikali
itaridhia waendelee kuwepo pale hilo halitajirudi tena tukishafanya maamuzi hatutarajii
kuona kutakuwa na maeneo ya urasimishaji au kuridhia kumega maeneo”Alisema
Waziri Dkt Mabula.

Awali
akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alianza kwa
kumpongeza Waziri Dkt Mabula huku akieleza mkoa wa Tanga wameshaanza kupambana
na migogoro ya ardhi kutokana na uwepo wa ushirikiano mzuri baina yao na Kamishna
wa Ardhi na watu wake wanawasaidia sana.

Alisema siri
moja wanawasaidia kwa sababu wanapokwenda kwake anawaambie wasimumunye maneno
kwani wao sio wanasiasa,wao wakija waniambia jambo hili lipoje historia yake na
kuna maeneo mengine kuna onekana kuna siasa na kuna maeneo maamuzi yanaonekana ni
eneo la siasa.

Mkuu huyo wa
mkoa alisema  lakini ikienda unakuta kuna
vijiji vimeanzishwa na serikali imepeleka huduma za muda mrefu ikiwemo shule za
Msingi,Hospitali hivyo wanapokwenda kuwaambia maeneo yao sio rasmi wanaanzisha
mgogoro na kuwatia watu wasiwasi.

“Lakini hayo
ndio umekuja na kamati kuyaondoa na hayo ni mambo makubwa yaliyofanywa na kamati
na ni mafanikio..Tanga na kuna maeneo ya muheza ya Mkonge yaliyokuwa rasmi ya
serikali watu wamevamia na katika kuvamia wenye umiliki hawakukemea jambo hilo
miaka sita au tano iliyopita  sasa
wanakuja kufata matumizi yake ya maeneo yao”Alisema

Aidha
alitolea mfano eneo la uwanja wa ndege kuna watu wameingia kuna mipaka na kuna
watu wameingia na kutaka kuipeleka serikali mahakamani na sasa hawana ndege
kubwa kutokana na uwepo wa mgogoro na wananchi.

“Sasa
tumewaachia miaka 10 serikali nimeambiwa mtaingia kwenye ukarabati  wanatafakari tunaomba huo mgogoro umalizike
mapema ili mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege uendelee na kufungua
fursa”Alisema

Naye kwa upande
wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi alisema kamati hiyo imepita
maeneo mbalimbali na kuweza kutoa mrejesho wa maamuzi ya baraza la mawaziri
kuhusu migogoro iliyopo kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Alisema baada
ya kutolewa maamuzi hayo ilikubaliana kamati hiyo ya mawaziri nane ipite nchi
nzima kueleza nini kimeamuliwa kwa migogoro hiyo ambayo ipo muda mrefu na
imekuwa ni kero kwa wananchi.

About the author

mzalendoeditor