Featured Kitaifa

RAIS SAMIA: HESHIMA YA UOGA ILIKUZWA SABABU KULIKUWA NA ‘SIMBA WA YUDA’

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Mawaziri pamoja na Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

……………………………………………………………..

Rais Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi Watule leo Aprili 2, 2022 amesema “Tunasifiwa kwamba maboresho tuliyoyafanya Awamu ya Tano yamekuza heshima ndani ya Utumishi wa Umma.

Heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na ‘Simba wa Yuda’ ambaye ulikuwa ukimgusa sharubu anakurarua”

Rais ameongeza “Hata hivyo hatukukua kivile. Heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie. Hicho ndicho tunachokosa Serikalini”

Aidha, Rais amesema Serikali itaimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kiendelee kufundisha watu majukumu ya Utumishi wa Umma. Amelitaka Baraza la Maadili lisimame kwenye Sheria na kurekebisha Maadili ya Watenda kazi wa Tanzania

About the author

mzalendoeditor