Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Damas Daniel Ndumbaro (Mb) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Pindi Hazara Chana (Mb) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Jaji Mstaafu Ibrahim Mipawa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Peter Ilomo kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Suzan Mlawi kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 02 Aprili 2022.

Viongozi Walioapishwa Wakila Kiapo cha Maadili, kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Mawaziri pamoja na Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Maadili katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Daniel Ndumbaro (Mb) pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Pindi Hazara Chana mara baada ya hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Jaji Mstaafu Ibrahim Mipawa, Peter Ilomo Mjumbe wa Baraza la Maadili na Suzan Mlawi Mjumbe wa Baraza la Maadili, kwenye hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 02 Aprili 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. PICHA NA IKULU

…………………………………………………………………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kufanya kazi kwa kuzingatia Mipango, Sheria, Miongozo, pamoja na Dira ya Maendeleo ya nchi ili kukuza ustawi wa taifa.

Mhe. Rais Samia amesema hayo leo mara baada ya kuwaapisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili pamoja na Wajumbe wake wawili na viongozi wengine pia katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa nchi baada ya kuathiriwa na UVIKO 19, hivyo ili kufikia azma hiyo ni wajibu kila Kiongozi kwenye kila sekta kutekeleza wajibu na majukumu yake ipasavyo.

Rais Samia amewataka Viongozi hao kusimamia na kutekeleza majukumu waliyopangiwa kikamilifu kwa kushirikiana, kuheshimiana na kuzingatia viapo vyao.

Kwa upande wa Baraza la Maadili, Rais Samia amewataka viongozi aliowaapisha kuanza kazi mara moja kwa kuzifanyia kazi kesi za maadili ndani ya Utumishi wa Umma zinazowasilishwa katika Baraza hilo.

Hafla hiyo ya Uapisho imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Katanga pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Previous articleDKT.MPANGO AZINDUA MBIO ZA MWENGE 2022,AIAGIZA TAKUKURU KUKAMILISHA UCHUNGUZI WA MIRADI 52
Next articleRAIS SAMIA: HESHIMA YA UOGA ILIKUZWA SABABU KULIKUWA NA ‘SIMBA WA YUDA’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here