Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab, marehemu Fatma Binti Baraka almaarufu Bi Kidude, amepewa tuzo ya heshima katika shughuli ya utoaji wa Tuzo za Tanzania Music Awards, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Wengine waliopewa tuzo za heshima, ni marehemu Ruge Mutahaba na msanii Diamond Platnumz kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika tasnia ya muziki nchini. Ruge ameenziwa kwa kuanzisha kituo cha THT (Tanzania House of Talents) kilichozalisha wasanii wengi na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya muziki Tanzania.
Diamond amepewa heshima hiyo kwa sababu ni msanii wa muziki aliyeleta mabadiliko kwa kuongeza thamani ya muziki nchini na amefanya hivyo kwa kuweka viwango vya malipo kuuza sanaa nje ya nchi na kutangaza kiswahili nje ya nchi.
Pia kwa kutoa ajira kwa vijana, kuchangia maendeleo ya uchumi kwa kulipa kodi.