Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameshiriki mafunzo kuhusu Mfumo wa Msamaha wa Kodi katika Miradi ya Maendeleo. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mhandisi Kemikimba amesema mfumo huo utasaidia zaidi katika utekelezaji wa miradi ya maji hapa nchini.
Pamoja na mafunzo, amewataka wataalamu wa TRA kufuatilia utekelezaji wa mafunzo hayo katika kazi.