Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA ATAKA WADAU WA ELIMU NCHINI KUIPITIA SERA YA ELIMU YA MWAKA 2014 NA KUTOA MAONI NINI KIBORESHWE

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika leo Machi 30,2022 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda,akisisitiza jambo kwa wadau wakati wa mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika leo Machi 30,2022 jijini Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Carolyne Nombo,akiwapongeza wadau walioshiriki katika mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika leo Machi 30,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba,akizungumza  wakati wa mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika leo Machi 30,2022 jijini Dodoma.

KAMISHNA wa Elimu nchini Dkt.Lyabwene Mtahabwa,akielezea namna wanavyoendelea kupokea maoni ya wadau wakati wa mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika leo Machi 30,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali  wakati wa mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi uliofanyika leo Machi 30,2022 jijini Dodoma.

……………………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amewataka wadau wa elimu nchini kuipitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na kutoa maoni yatakayowezesha serikali kuandaa au uboresha Sera hiyo ambao unakwenda sambamba na uboreshaji wa mitaala ya elimu.

Waziri Mkenda ametoa wito huo leo Machi 30,2022 jijini Dodoma wakati  wa mkutano wa kupokea maoni kuhusu uboreshaji wa mitaala na sera ya elimu kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja na wamiliki wa shule binafsi.

Amesema  kama nchi tayari inayo sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo inamajibu mengi ya maswali yanayoibuka kuhusu ubora wa elimu inayotolewa hapa nchi.

“Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inahitaji kufanyiwa mapitio ili iweze kuendana na mazingira ya sasa na iweze kutekelezeka,” amesema Prof. Mkenda.

Aidha Waziri Mkenda amesema kuwa ameunda kamati ya wataalamu ili wakafanyie mapitio sera hiyo ili kujua ni kwanini sera haitekelezwi tangu ilipopitishwa mwaka 2014 ambayo inamajibu mengi ya maswali yanayoendelea kuibuka kuhusu ubora wa elimu yetu.

Prof.Mkeda amesema kuwa lengo la serikali ni kuwa na sera itakayoakisi mahitaji halisi ya ubora wa elimu na amebainisha kuwa mwezi wa tano mwaka huu 2022 wanatarajia kupokea rasimu ya mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa elimu namna ya kuboresha elimu hapa nchini.

“Ukiangalia mapendekezo ya wadau wengi ni wanataka elimu ya lazima iwe miaka 10 na Sera yetu ya mwaka 2014 inataka mwanafunzi mara baada ya kupata elimu ya awali inatakiwa apate elimu ya lazima kwa miaka 10 ili kumuwezesha mwanafunzi kujua kusoma, kuandika kuhesabu na kupata maarifa ujuzi ya elimu ya ufundi stadi” amesema.

Awali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo amewashukuru Viongozi wa Dini na Wamiliki wa Shule binafsi kwa kushiriki katika mkutano huo muhimu wa kutoa maoni ambayo yatasaidia kuboresha Sera na Mitaala ili watoto wa Kitanzania wapate elimu itakayowapatia ujuzi na kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania.

Kwa upande wake Kamishna wa Elimu nchini Dkt.Lyabwene Mtahabwa, amesema mpaka sasa serikali imepokea maoni ya wadau mbalimbali laki moja na elfu mbili ya namna wanavyopendekeza elimu inayotolewa hapa nchini iweje.

Dk.Mtahabwa amesema miongoni mwa maoni hayo ni kuondoa maudhui yanayojirudia rudia kwa wanafunzi mara baada ya kuvuka darasa, kutoa ujuzi kwa wanafunzi kulingana na geografia ya maeneo na fulsa za kiuchumi zinazopatikana eneo husika.

Mengine ni lugha ya kujifunza na kujifunzia na kuwekwa kwa msisitizo wa maadili mema tangu mwanafunzi akiwa mdogo kabisa ili kuepuka mmomonyoko wa maadili bili kusisitiza elimu ya kawaida pekee.

Naye  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba amesema kuwa maboresho ya mitaala unashirikisha makundi yote na katika kuboresha sera ya elimu na mitaa wanajifunza pia kupitia nchi zilizofanikiwa zaidi kuona namna wanavyoendesha elimu yao.

”Zoezi la kupokea maoni litaendelea hata kipindi ambapo sera na mitaala itapitishwa lakini wataendelea kupokea maoni na maoni hayo yatakuwa yanaboresha sera na mitaala kadri itakavyokuwa inahitajika”ameeleza Dk.Komba

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Dini na wamiliki wa shule wamesema elimu ni msingi wa kila kitu hivyo pamoja na mambo mengine umakini kwenye lugha ya kufundishia unahitajika kwa kuhakikisha lugha ya Kiswahili na Kingereza zinatumika.

About the author

mzalendoeditor