Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandishi Anthony Sanga akizungumza na Kamati ya wataalam kutoka sekta mbalimbali zinazohusika katika utekelezaji wa mradi wa maji Simiyu. Wataalam kutoka sekta mbalimbali zinazohusika katika utekelezaji wa mradi wakijadili masuala mbalimbali kuhusiana na utekelezaji wa mradi. 

Picha ya pamoja na wataalam na wadau wa sekta mbalimbali zinazohusika katika utekelezaji wa mradi

***************************

Serikali kwa kushirikiana na Benki ya KfW kwa niaba ya Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund – GCF) inatekeleza mradi wa kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabia nchi katika Wilaya tano (5) za Mkoa wa Simiyu ambazo ni Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu. Katika awamu ya kwanza mradi wa maji utatekelezwa katika Wilaya za Busega, Itilima na Bariadi.

Akizungumza na Kamati ya Wataamu wa Sekta mtambuka, jijini Dodoma Machi 29, 2022 Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandishi Anthony Sanga amesema maandalizi ya kuanza utekelezaji wa mradi zinakwenda vizuri na kwamba wako katika hatua za mwisho za kuanza utekelezaji.

Mradi huo unakadiriwa kugharimu jumla ya kiasi cha EURO Milioni 171, ambapo GCF watachangia EURO Milioni 102.7, Benki ya KfW itachangia EURO Milioni 26.1, Serikali ya Tanzania EURO Milioni 40.7 na Wananchi kupitia nguvu zao watachangia EURO Milioni 1.5. Hadi mwezi Februari 2022, awamu ya kwanza ya fidia kiasi cha shilingi 1,519,074,522.16 kimelipwa kwa wananchi wapatao 1,201 kati ya 1,308 walio tathiminiwa. Aidha, taratibu za kuwapata wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi zipo katika hatua za mwisho.

Previous articleWAZIRI MKUU MAJALIWA ATETA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI AUSTRIA
Next articleWAZIRI MKENDA ATAKA WADAU WA ELIMU NCHINI KUIPITIA SERA YA ELIMU YA MWAKA 2014 NA KUTOA MAONI NINI KIBORESHWE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here