Featured Kitaifa

MBUNGE KOKA AIPIGA JEKI UVCCM KATA YA KONGOWE

Written by mzalendoeditor

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akimkabidhi viti 25 vya plastiki kiongozi wa UVCCM Kata ya Kongowe ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake katika kuwasaidia vijana kuweza kuanzisha miradi yao wenyewe.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini wa Kulia akikabidhiwa cheti cha pongezi na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kongowe Saimon Mberwa ikiwa ni kwa ajili ya kumpongeza kwa juhudi zake anazozifanya katika kukipigania chama.

…………………………………………………

Na Victor Masangu, Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za chama cha mapinduzi (CCM) katika kuleta chachu ya maendeleo ametekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kutoa viti vipatavyo 25 vya plastiki kwa ajili ya kuanzisha mradi wa umoja wa vijana kata ya Kongowe (UVCCM) ambao utawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Koka amekabidhi viti hivyo  vyenye thamani ya kiasi  cha shilingi laki nne na nusu  wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa CCM kata ya Kongowe ambao ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa matawi pamoja na ngazi ya Kata.

Alisema kwamba ameamua kusapoti juhudi ambazo zinafanywa na vijana wa CCM Kata ya Kongowe na ndio maana ameamua kutoa viti hivyo ikiwa ni ahadi yake ya kuwasaidia vijana kuanzisha mradi wa kukodisha viti ambao pia utakuwa ni fursa kwao katika suala zima la kujiongezea kipato na kuwataka wawe waadilifu katika kukijenga chama.

Pia katika mkutano huo Koka aliweza kukabidhiwa cheti  cha pongezi na Chama cha mapinduzi kata ya kongowe (CCM)   kwa ajili ya mchango wake ambapo pia aliweza naye kugawa vyeti mbali mbali kwa viongozi wa cham ahicho ambao wameweza kufanya kazi  zao vizuri katika kipindi kirefu kwa mafanikio makubwa.

Pia Koka katika hatua nyingine aliwataka wanachama wa CCM katika kuelekea katika chaguzi kuhakikisha wanachukua fomu kwa ajili ya kugombea na kuachana na tabia ya wote lengo ikiwa ni kushirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kuweza kukijenga chama kiweze kutekeleza ilani kwa vitendo na kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.

Aidha Mbunge huyo aliwawataka wanachama hao kuachana kabisa na vitendo vya kuwa na makundi ambayo  yanasababisha  kupotea  kwa  umoja na kwamba wahakikishe kuwa wanashiriki katika vikao mbali mbali vya chama ili kujadili mambo mbali mbali ya kuwaletea wananchi maendeleo katika Nyanja mbali mbali.

“Makundi ndani ya Chama chetu cha mapinduzi kwa kweli hayafai kabisa hata kidogo kwa hiyo kitu kikubwa kwa upande wangu mm uwa sipendelei katika kuwa na makundi na ndio maana nilipochaguliwa kuwa Mbunge wenu wa jimbo la Kibaha ninakuwa ni kiongozi wa wananchi  wote bila ya kuwa na makundi na pia kitu kingine tunaelekea kwenye uchaguzi kwa hivyo kila mwanachama ana haki ya kugombea tujitokeze kwa wingi,”alisema Koka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya kongowe Saimon Mbwerwa alimpongeza Mbunge huyo kwa kuweza kutoa viti hivyo ambavyo vitaweza kuwasaidia   vijana wa  UVCCM  kata ya kongowe kuweza kutimiza malengo yao ambayo wamejiwekea katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kujiiingizia kipato.

“Tumefanya mkutano wetu mkuu wa Kataya kongowe lakini napenda kutoa shukrani zangu za kipekee kwa Mbunge wetu kwa kuweza kuonyesha ushirikiano wake katika mkutano huu pamoja na kutimiza ahadi yake ya kuweza kutoa viti vya plastiki vipatavyo 25 hii kwa kweli ni hatua nzuri katika kukijenga chama chetu  kuanzia ngazi  za chini hadi za juu na kwamba nawashukuru viongozi wangu wote wa kata kwa kufanikisha mkutano huu,”alisema Mberwa.

Nao baadhi ya wanachama wakongwe wa CCM ambao walihudhulia katika mkutano huo walisema kwamba Mbunge wao amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia mambo mbali mbali ikiwemo suala la maendeleo kwa wananchi katika  miradi ambayo inakuwa inaanzishwa amekuwa akichangia kwa kiasi kikubwa.

“Kwa kweli Mbunge wetu wa jimbo la Kibaha mjini mheshimiwa Silvestry Koka ni mtu mwenye kushirikiana na wananchi katika miradi mbali mbali ya maendeleo na kwamba ata ukiwa na shida amekuwa mstari wa mbele katika kusikiliza kero na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wananchi wake na huu ni mfano wa  kuigwa na watu wengine kwanai amefanya mengi mazuri,”alisema

Pia waliongeza kuwa Mbunge huyo ameweza kutoa sapoti kubwa kwa wanachama wa wa CCM katika ngazi zote za matawi hadi Kata na kwamba alishatoa pikipiki katika kata zote pamoja na kutoa simu janja kwa kata zote 14 amabzo zitaweza kutumika katika kuwasajilia wanachama kwa njia ya kieletroniki pamoja na kusaidia miradi mingine katika sekta ya afya pamoja na elimu.

About the author

mzalendoeditor