Featured Kitaifa

UKAME WAUA MIFUGO 92,047 SIMANJIRO

Written by mzalendoeditor

Aliyeko katikati ni Afisa mabadiliko ya tabia ya nchi ,Gidion Sanago kutoka Pingo’s Forum aliyeko kushoto kwake ni Afisa Jinsia Nailejileji Tipap na Mwanasheria wa Pingo’s Forum Saitoti Parmelo wakizungumzia juu ya utafiti huo.(Happy Lazaro)
……………………………………..
Happy Lazaro,Arusha
Arusha .Kutokana na kuwepo kwa athari za mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo mbalimbali nchini  na kusababisha ukame pamoja na vifo vya mifugo , wilayani Simanjiro jumla ya mifugo 92,047  imeripotiwa kufa kutokana na  mabadiliko hayo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Afisa Kilimo na Mifugo,Dk Swaleeh Masaza  katika uzinduzi wa utafiti juu ya uwezo wa jamii za  kifugaji kukabiliana na majanga,ambapo amesema kati ya mifugo  hiyo ng’ombe waliofariki ni  46,028.
Amesema kuwa, Kondoo 21,046 walifariki,Mbuzi 21,070 na Punda 2003 hata hivyo,elimu ya asili iliyopo katika jamii hizo imesaidia sana kupunguza athari zaidi.
Naye Mtafiti wa masuala ya mazingira Enock Changula amesema katika utafiti uliofanywa katika vijiji vitano wilaya ya Simanjiro umebaini elimu ya asili imesaidia sana jamii ya kifugaji kukabiliana na majanga.
Ameongeza kuwa,elimu hiyo imesaidia jamii kukabiliana pia na magonjwa, Mafuriko lakini pia upatikanaji wa habari na kupashana habari.
Amefafanua kuwa,mfumo wa wafugaji kuhamahama umeonekana kuwa na faida katika utunzaji wa mazingira lakini pia unawezesha kuboresha ardhi ambayo imekuwa kivutio cha wanyamapori .
Afisa mabadiliko ya tabia nchi  na mazingira wa shirika la  PINGOS Forums Gidion Sanago amesema utafiti huo umebainisha umuhimu wa kutambulika,kulindwa na kuendelezwa elimu ya asili katika kukabiliana na majanga.
Hate hivyo aliwaomba watungaji wa sera waanze kuthamini,kutambua na kuingiza  elimu hiyo katika utungaji  sera za nchi.

Afisa wa jinsia na maendeleo ya jamii wa PINGOS Forums,Nailejileji Tipap amesema wahanga wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake na watoto,hivyi elimu ya asili imeweza kutumika katika kukabiliana na majanga hata magonjwa ya akina mama na watoto.

About the author

mzalendoeditor