Msanii wa filamu na mchekeshaji Steven Nyerere Ijumaa Machi 25, 2022 ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania(SMT).
Steve ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais na shirikisho hilo wakati wote, na amesema kuwa licha ya kujiuzulu nafasi hiyo ataendelea kuwepo kwenye maisha ya Wasanii kwani bado ana nafasi za uongozi sehemu mbalimbali na ataendelea kuendesha matamasha yanayowahusu Wasanii.