Featured Kitaifa

MWANAMKE AUWAWA MCHANA KWEUPE TABORA

Written by mzalendoeditor

Na Lucas Raphael Tabora

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Leah Emanuel Ndaki (27) ameuwawa kikatili na watu wasiojulikana baada ya kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake mchana kweupe akiwa nyumbani kwake .

Akizungumzia tukio hilo mbele ya  waandishi wa habari jana Kamamda wa polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea machi 22 mwaka huu majira ya saa nane mchana.

Alisema kwamba mauaji hiyo yalifanyika  katika  mtaa wa mtakuja kata ya malolo manipaa ya Tabora wilaya ya Tabora mkoani humo.

Kamanda Abwao alisema mbinu iliyotumika ni kumvizia na kumshambulia akiwa nyumbani kwake  ndipo mtu au watu waliweza kumchoma na kitu chenye ncha kali na kusababisha damu nyingi kumtoka na kupelekea kifo chake

Kamanda huyo wa Polisi alisema kwamba jeshi hilo linafanya juhudi za kubaini chanzo cha tukio hilo pamoja na kumpata mtuhumiwa ama watuhumiwa walifanya mauaji hayo.

Alisema kwamba jeshi la polisi alitaacha mpaka mtuhumiwa huyo aweze kupatikana ili aweze kukabiliana na mkono wa sheria na  iwe fundisho wa watuhumiwa wa aina yake .

Kamanda Abwao alitoa Rai kwa wananchi mkoani Tabora kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kuendelea kutoa Taarifa mbalimbali za kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu na kuongeza kwamba wananchi wasisite kutoa taarifa walizonazo ili kufanya wapesi kwa  jeshi la polisi kuwakamata wahalifu.

About the author

mzalendoeditor