Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo tarehe 24 Machi,2022, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Nchini, Mhe. Balozi Hussain Ahmad Al Homaid Jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao pamoja na mambo mengine wamezungumzia ushirikiano wa Nchi hizo mbili katika kuimarisha na kuongeza fursa za Elimu nchini.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza.

Previous articleMFUMO WA KIELETRONIKI WA TATHMINI YA HALI YA WATUMISHI WAZINDULIWA JIJINI DODOMA
Next articleWAZIRI NAPE AKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here