Uncategorized

SH.BILIONI 26 ZAKAMILISHA UJENZI WA STENDI YA NYAMHONGOLO

Written by mzalendoeditor

Na Asila Twaha, Ilemela

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Zedi amezishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati yenye manufaa kwa nchi.

Mhe. Zedi aliyasema hayo  katika ziara ya Kamati hiyo yenye lengo la kukagua fedha za Umma zinazopelekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo kamati hiyo ilikagua miradi 3 ukiwemo mradi wa kimkakati wa ujenzi wa stendi ya kisasa Nyamhongolo, ujenzi wa Jengo la Utawala na ufuatiliaji umiliki wa hisa katika Rock City Mall.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw. Joseph Apolinary amesema, mradi wa stendi Nyamhongolo mpaka sasa umekamilika kwa 100% na mpaka kukamilika kwakwe umegharimu shilingi bilioni 26 lakini makadirio ya awali ya mradi yalikuwa shilingi bilioni 28 lakini kutokana na usimamizi wa ujenzi waliweza kutumia shilingi bilioni 26.

Amesema ujenzi wa stendi ya Nyamhongolo utakuwa ni chanzo cha ongenzeko la mapato kwenye Halmashauri hiyo ambapo majengo yaliyojengwa miundombinu ya benki, eneo la kuegesha magari(parking) yenye uwezo wa kuogesha malori, mabasi, magari binafsi, bodaboda na bajaji, maduka makubwa na madogo, maeneo ya wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa lakini pia kuna hosteli ambapo itaweza kupokea abiria wanaoendelea na safari, wageni wa nje na maderava ambapo amesema hivyo vyote ni vyanzo vya mapato.

“Mradi wa stendi hii umetoa fursa na kutangaza nafasi kwa wananchi watakaohitaji kukodisha maduka ya kufanya biashara katika eneo hili tumetangaza kwenye vyombo vya habari mbalimbali na mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 29 Machi, 2022” amesema Apolinary

Ameendelea kufafanua mbali ya mradi huo kuwa na mahitaji yote muhimu lakini pia amesema, umezingatia upatikani mzuri wa miundombinu maji na umeme.

Kwa upande wake, mjumbe wa Kamati Mhe. Tauhida Cassian ameushauri uongozi wa Ilemela kudhibiti tabia ya baadhi ya watendaji kujimilikisha maduka na baadae kuwakodishia wananchi kwa kiasi kikubwa cha fedha amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Robert Gabriel kusimamia suala hilo kwa kufuata sheria na taratibu katika utoaji wa nafasi kwa wananchi ili kwa mtu mwenye sifa apatiwe ili waweze kufanya biashara.

Aidha, Mhe. Zedi amesema, ujenzi wa stendi hiyo ya kisasa ni mfano wa kuigwa kwa Halmashauri zilizoandika andiko la kuomba mradi wa ujenzi wa stendi amezishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kutembelea stendi hiyo ili kujifunza na kuwa na miradi bora ya kimkakati katika Halmashauri zao.

Mtaalam mshauri na usimamizi wa ujenzi wa stendi hiyo alikuwa ni (BICO) kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na mkandarasi ni kampuni kutoka China (Stecol Cooperation).

About the author

mzalendoeditor