MWANAMKE mwenye umri wa miaka 38 raia wa Ghana Elizabeth Amoaa, ameieleza BBC kuwa akiwa na miaka 32 daktari aligundua kuwa ana mifuko miwili ya uzazi na njia mbili za uzazi ikiwemo sehemu mbili za jinsia ya kike.
Amesema kuwa awali kabla ya kugundua tatizo hilo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa miaka mingi ambayo mara nyingi yalimfanya ashindwe kufanya kazi
Elizabeth ambaye kwa sasa anaishi Uingereza anasema hali hii ni ya asili tu mtu anazaliwa nao na aliwahi kupata ujauzito hapo awali.
“Ninaweza kuwa mjamzito katika tumbo langu la kulia na bado kupata hedhi kupitia kushoto kwangu. Ndiyo maana nilipokuwa na ujauzito wa binti yangu nilikuwa nikiona damu,” aliiambia BBC.
CHANZO:BBSSWAHILI