Featured Michezo

TANZANIA YAICHAPA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI MECHI YA KIRAFIKI

Written by mzalendoeditor

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mechi ambayo ilichezwa kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa.

Taifa Stars ilianza kupata bao la mapema kabisa kupitia kwa kiungo Novatus Dismas aliepiga faulo moja kwa moja na kutinga nyavuni dakika ya 10 ya mchezo.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake tumeshuhudia wachezaji wageni wakionesha umahiri wao na kumkosha kocha wa Kim Poulsen.

Taifa Stars ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ambapo mabadiliko hayo yalizaa matunda ambapo Faridi Musa aliweza kutengeneza bao la pili lilofungwa na mshambuliaji Mbwana Samata dakika ya 63 ya mchezo.

George Mpole ndiye aliweza kumalizia msumali wa mwisho mara baadaa ya kuingi dakika za nyongeza na kufanikiwa kupachika bao zuri akipokea pasi kutoka kwa kiungo Simon Msuva dakika ya 93 ya mchezo mara baada ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati   kupata goli la kufuta machozi na matokeo kuwa 3_1.

About the author

mzalendoeditor