Featured Kitaifa

WANAWAKE UCSAF WATOA MSAADA HOSPITALI YA MIREMBE JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi.Justina Mashiba ,akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa vyakula mbalimbali na maboksi ya taulo za kike katika Hospitali Kuu ya Afya ya Akili Mirembe vyenye thamani ya fedha za Kitanzania sh Milioni 3.5 leo Machi 22,2022 jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi.Justina Mashiba,akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Lawala (mwenye miwani katikati) msaada wa vyakula mbalimbali na maboksi ya taulo za kike katika Hospitali Kuu ya Afya ya Akili Mirembe vyenye thamani ya fedha za Kitanzania sh Milioni 3.5 leo Machi 22,2022 jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi.Justina Mashiba akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula mbalimbali na maboksi ya taulo za kike katika Hospitali Kuu ya Afya ya Akili Mirembe vyenye thamani ya fedha za Kitanzania sh Milioni 3.5 leo Machi 22,2022 jijini Dodoma.

…………………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WANAWAKE wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF wamekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali na maboksi ya taulo za kike katika Hospitali Kuu ya Afya ya Akili Mirembe vyenye thamani ya fedha za Kitanzania sh Milioni 3.5.

Akikabidhi msaada huo Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Bi.Justina Mashiba  amesema kuwa UCSAF ni Taassi ya Serikali na majukumu yao makubwa ni kupeleka mawasiliano vijijini.

Amesema wamekwenda kutoa msaada katika hospitali ya Mirembe na kuwasalimia wagonjwa waliopo hospitalini hapo Kama njia mojawapo ya kurudisha walichojaaliwa katika jamii.

“Hasa ukizingatia mwezi Machi ni mwezi wa wanawake na tumeadhimisha nakusherekea Siku ya wanawake hivyo tumeona ni busara kuleta kitu kidogo tulichonacho kwaajili ya kuwasaidia ndugu zetu waliopo hospitalini hapo wakipatiwa matibabu,”amesema Mashiba.

”Sisi kama wanawake tuliopo serikalini tumeona ni vizuri kutoa kidogo tulichonacho kwa ajili ya wenzetu hawa wanaopatiwa matibabu hospitalini hapa mirembe na yote ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutuvusha salama na kuingia mwaka mpya na kusherekea katika maadhimisho ya Siku ya wanawake, kama tuliweza kufurahi basi na wezetu walioko hapa nawao waweze kufurahi,”amesisitiza

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Lawala,amewashukuru UCSAF kwa msaada wa Sukari ,Mafuta ,Maharage Mchele na taulo za kike wameonyesha ni jinsi gani wanawajali.

“Nawashuruku sana kwa hatua mliyo ifikia mmeamua kuja kushirikiana na sisi na kwa kweli Mungu awabariki kwa hiki mlicho kitoa kizidi kuwaletea neema zaidi kweli tumefurahi na tutazidi kuwashukuru UCSAF ” Amesema Dk.Lawala

 Mhasibu kutoka UCSF Nadia Amir,amesema wamefurahi kuwa hapo na kutoa kidogo walichopata kwaajili ya jamii hasa wagonjwa wanaopatiwa matibabu Hospitali ya mirembe Kama sehemu ya maadhimisho hayo.

” Nawapongeza Sana Uongozi wa hospitali ya Mirembe na Uongozi wa (UCSAF) kwa kushirikiana pamoja katika kuhakikisha Siku hiyo inafanikisha tunashukuru kuwa hapa na kutoa hiki tulichojaliwa.

Na kuongeza kuwa”Tumechagua mirembe tumeona hapa kunauhitaji Mkubwa lakini pia hapa ni nyumbani na UCSAF ipo Dodoma hivyo niseme wazi kutoka moyoni kama waafirika tunapitia maisha tofauti hivyo mtu akikosa tunakuja anavyojisikia kwa hiki kidogo tulichotoa tunajisikia ni wenye furaha,” amesema Muweka Hazina Nadia

Kwa upande wake Katibu wa Afya Hospitali ya Mirembe Jackson Mjinja amewashukuru UCSAF kuwapelekea matendo hayo ya huruma na kuomba na watu wengine waguswe kupeleka misaada kamaa hiyo kwani huitaji ni Mkubwa hususani kwa wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili.

Amesema Hospitali ya Mirembe imegawanyika katika sehemu kuu nne, ambapo kuna Mirembe yenyewe Hospitali kuu wagonjwa wakawaida eneo la Isanga wagonjwa Wa akili na wenye kesi 234, eneo la Itega ni wagonjwa wa akili walioathirika na Madawa ya kulevya 524 ,Hombolo kilimo na ufugaji na waliotelekezwa na jamii wapo 6 lakini pia kuna eneo lao la Annex kwaajili ya miradi ya Hospitali.

“Tunatoa shukrani kwa mkurugenzi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Hospitali ya Mirembe kwa mashirikianao mazuri na kuhakikisha kuleta misaada hasa katika kusherehe yao Siku ya wanawake na kutukumbuka sisi Mirembe,”amesema  Mjinja.

About the author

mzalendoeditor