Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA IHUISHAJI NA UIMARISHAJI WA MFUMO WA USAMBAZAJI WA MAJI ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya ujenzi wa Mradi wa Matangi ya Maji Safi na Salama Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa Mfumo wa Usambazaji Maji Zanzibar,ikiwa ni Wiki ya Maji Duniani,(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid.

WANANCHI wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa Mfumo wa Usambazaji wa Maji Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu (ZAWA) Dkt. Salha Mohamed Kassim, akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Matangi ya Maji Safi na Salama Kwarara Kidutani, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa Mfumo wa Usambazaji Maji Zanzibar, ikiwa ni Wiki ya Maji Duniani.(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe. Shaib Kaduara.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa kitambaa kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa Mfumo wa Usambazaji Maji Zanzibar,na (kushoto kwa Rais)Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar. Mhe Shaib.Kaduara akiwa na Viongozi wa Wizara na ZAWA wakishiriki kuondoa kitambaa,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mradi huo Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja, ikiwa sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.,Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa Mfumo wa Usambazaji Maji Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ujenzi wa matangi ya maji ya Mradi huo Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharini “B” Unguja ikiwa sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum na Mwakilishi wa Kampuni ya L&T Construction Bw.Hari Prakash, (kushoto kwa Rais) baada ya kumalizika kwa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa Mfumo wa Usambazaji wa Maji Zanzibar, mradi huo wa ujenzi wa matangi ya maji katika eneo la Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

About the author

mzalendoeditor