Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limesema linamshikilia mtoto mmoja (Jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa mtaa wa Kihesa Kilolo ‘B’ katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wenzie 19 kwa nyakati tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema taarifa za awali zilionyesha mtuhumiwa huyo alikuwa amewafanyia vitendo vya ulawiti watoto wenzie 3 lakini baada ya uchunguzi wa Jeshi hilo imebainika sasa idadi ya waathirika wa vitendo hivyo vya ulawiti ni 19 huku taarifa zikionyesha mtuhumiwa huyo alikuwa akiwarubuni watoto wenzie kwa kuwapa vitu vidogo vidogo ikiwemo pipi na juice.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CCM) Dk. Jesca Msambatavangu amesema ofisi yake imeanzisha ushirikano wa karibu na Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia ktk kuhakikisha inatoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya malezi ya watoto ili kukomesha vitendo vya ubakaji na ulawiti.

Previous articleMAKAMU WA RAIS ATETA NA BALOZI WA TZ NCHINI AUSTRIA
Next articleRAIS DK.MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA IHUISHAJI NA UIMARISHAJI WA MFUMO WA USAMBAZAJI WA MAJI ZANZIBAR

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here