Featured Kitaifa

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA BOUYGUES WAJADILI UKARABATI WA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS KAMBARAGE NYERERE 

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Bougues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa Bw. Eric Fleurisson, baada ya mazungumzo yaliyofanyika wizarani hapo, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Bouygues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa Bw. Eric Fleurisson (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa nchi hizo mbili baada ya kukamilika kwa mazungumzo jijini Dodoma. Kushoto ni Dennis Keener wa Kampuni ya Kimataifa ya Bouygues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa, Wa pili Kulia ni Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine na wa kwanza kulia ni Mchumi Mkuu Idara ya Mipango ya Kitaifa Bw. Charles Lumaze.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao na ujumbe kutoka wa Kampuni ya Kimataifa ya Bougues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Bouygues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa Bw. Eric Fleurisson, akizungumza wakati alipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), jijini Dodoma.

Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine (Kushoto), na Mchumi Mkuu Idara ya Mipango Ya Kitaifa Bw. Charles Lumaze, wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na ujumbe kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Bouygues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

………………………………………….

Na. Ramadhani Kissimba, WFM, Dodoma

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Bouyges Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa ambayo hivi karibuni iliingia makubaliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jengo la pili (terminal II).

Akizungumza katika majadiliano hayo yaliyofanyika Jijini Dodoma, Mhe. Nchemba alisema Wizara ya Fedha na Mipango iliona ni vyema kukutana na kujadili namna ya kuanza mara moja shughuli hiyo ambayo utiaji sahihi wake ulifanyika nchini Ufaransa mwezi Februari,2022 na kushuhudiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais wa Ufaransa Mhe. Emmanuel Macron.

Mhe. Mwigulu aliuhakikishia ujumbe huo kuwa Wizara kupitia timu ya wataalam wake itakuwa tayari kwenda sambamba kwenye kila hatua kwa upande wa maandiko ya kitaalamu hasa kwenye hatua ya usanifu wa mradi na taratibu zote zitakapokamilika kusiwe na muda mrefu wa uchambuzi wa mradi ili utekelezaji wake uweze kuanza mara moja.

‘’Timu yetu ya wataalam itakuwa tayari kwenda sambamba nanyi, na pale mtakapokamilisha hatua ya usanifu wa mradi na mapendekezo kwa upande wa fedha tutakuwa pamoja kupitia Idara ya Usimamizi wa Madeni na Mipango ya Kitaifa ili kujua hatua mliyofia na kukamilisha taratibu zote ili kusiwe na ucheleweshaji wa mradi’’ Alisema Mhe.Mwigulu.

Mhe. Mwigulu aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa taratibu zote zikiwamo za kifedha zitakamilishwa kwa wakati ili mradi uweze kuanza mara moja kama Mhe. Rais alivyoagiza wakati wa ziara yake nchini Ufaransa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Bouygues Batiment (BBI) ya nchini Ufaransa Bw. Eric Fleurisson, alisema mradi wa ukarabati wa uwanja huo utashirikisha Makampuni ya ndani na utakapokamilika utakuwa uwanja wa kisasa zaidi na kuongeza uwezo wa kuhudumia safari za ndani na kufungua fursa kutumika na nchi Jirani na Tanzania, hivyo kuingizia nchi mapato kupitia fedha za kigeni.   

About the author

mzalendoeditor