Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YAKAGUA MRADI WA MAZINGIRA ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile akisikiliza maelezo kuhusu majiko sanifu yaliyotengenezwa kupitia Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) Matemwe Kijini wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Zanzibar leo Machi 18, 2022.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika mradi wa kutengeneza boti za uvuvi Matemwe ziara ya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) Zanzibar leo Machi 18, 2022 Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile akizungumza na wanufaika wa mradi wa kutengeneza majiko sanifu na sabuni kupitia Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) Matemwe Kijini wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Zanzibar leo Machi 18, 2022.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira ilipofika kukagua mradi wa kutengeneza majiko sanifu na sabuni kupitia Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) Matemwe Kijini wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Zanzibar leo Machi 18, 2022.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Dkt. Dadi Omar Shajaka akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa utengenezaji wa boti za uvuvi kupitia Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) Matemwe Kijini wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Zanzibar leo Machi 18, 2022

………………………………………………………

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) Zanzibar leo Machi 18, 2022.
 
Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati walikagua shughuli za utengenezaji wa majiko sanifu unaotekelezwa na vikundi vya Matemwe Kijini baada ya kupewa mafunzo kuhusu teknolojia banifu katika Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini.
 
Wajumbe wa kamati hiyo walikagua sehemu ya majiko sanifu 90 yaliyotengezwa ambapo lengo ni kupunguza matumizi makubwa ya kuni na mkaa na hivyo kupunguza uharibifu wa misitu kutokana na ukataji holela wa miti.
 
Pia wajumbe walipata fursa ya kukagua utekelezaji wa ununuzi wa boti sita za uvuvi ambapo mzabuni anatarajiwa kutengeneza boti sita zitakazonufaisha vikundi vya uvuvi na utengenezaji wa sabuni na vipodozi kwa washiriki 45 kutoka shehia tatu za Matemwe pamoja na ununuzi wa vifaa.
 
Akizungumza na wananchi walionufaika na mradi huo Matemwe Mbuyutende, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Kihenzile alisema kamati mbali na kushiriki katika kutunga sheria na kuisimamia Serikali pia ina wajibu wa kutembelea na kukagua miradi.
 
Awali mmoja wa wanufaika wa mradi wa utengezaji wa sabuni na vipodozi Bi. Tatu Omar Juma alipongeza Serikali kwa kuwapelekea mradi huo na kusema inasaidia kuhifadhi mazingira.
Alisema watu wengi wanafikiria kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni lakini baada ya kupata mafunzo hayo wanaweza kuihifadhi miti hiyo na kuitunza huku wakiitumia kwa kujipatia kipato kwa kutengeneza bidhaa hizo.
Usimamizi wa Mradi huu unaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) kwa niaba ya Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) na Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu utekelezaji wake kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Halmashauri za Wilaya husika.
Kwa upande wa Zanzibar Mradi wa EBARR unaratibiwa na Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kushirikiana na Baraza la Mji Kaskazini A – Unguja.
 

About the author

mzalendoeditor