Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amekutana na Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC), Bw. Collen Kelapile katika kikao kilicholenga kupata maelezo kabla ya kushiriki kikao cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika tarehe 18 Machi, 2022, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Tanzania inashiriki katika kikao hicho ikiwa ni Mwenyekiti wa Nchi Wazalishaji wa Madini ya Almasi Afrika ( ADPA).

Aidha, kikao hicho kinalenga kujadili namna bora za kutumia rasilimali katika nchi husika kuibua maendeleo jumuishi kwenye jamii ambazo maliasili hizo zinapatikana ili zisaidie kuleta amani na hatimaye kufikiwa maendeleo endelevu.

Kikao hicho kitafanyika chini ya mada isemayo “Maliasili Jamii yenye Amani na Maendeleo Endelevu”

Previous articleWALEMAVU SUMBAWANGA WAISHUKURU SERIKALI KWA MIKOPO
Next articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KUMBUKIZI YA JPM CHATO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here