Featured Michezo

MSHAMBULIAJI WA YANGA PRINCESS ASAJILIWA SWEDEN

Written by mzalendoeditor

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Princess, Aisha Masaka amesajiliwa na Klabu ya BK Häcken FF inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Sweden kwa makubaliano maalum na timu.

Katika Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Yanga Princess leo Machi 15, 2022 imeeleza kuwa nyota huyo anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Soka la Wanawake Tanzania kusajiliwa bila majaribio kwenye Ligi Kubwa za Wanawake Barani Ulaya.

BK Häcken FF ni Mabingwa wa Ligi Kuu Wanawake Sweden msimu wa 2020 na wamekuwa wakishiriki UEFA Champions League na msimu huu wametolewa na Manchester City.

About the author

mzalendoeditor