Featured Michezo

BIASHARA YAICHAPA 2-1 PRISONS MJINI MUSOMA

Written by mzalendoeditor

Biashara United wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
Mabao ya Biashara United yote yamefungwa na Deogratius Mafie dakika ya 26 na 34, wakati la Prisons limefungwa na Ezekiah Mwashindilindi dakika ya 68.
Kwa ushindi huo, Biashara inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 13, wakati Prisons inaendelea kushika mkia na pointi zake 13, baada ya wote kucheza mechi 18.

About the author

mzalendoeditor