Featured Michezo

WAZIRI WA ZANZIBAR MGENI RASMI SIMBA NA RSB BERKANE YA MOROCCO

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Omar Said Shaaban atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC dhidi ya RSB Berkane ya Morocco.

Mchezo huo wa Kundi D utafanyika Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni.
Mechi ya kwanza wiki iliyopita Berkane ilishinda 2-0 mjini Berkane na sasa ndio inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Simba na US Gendamarie ya Niger zenye pointi nne kila moja, wakati ASEC ya Ivory Cost yenye pointi tatu inashika mkia baada ya mechi tatu za awali.

About the author

mzalendoeditor