Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA ATETA NA WADAU BINAFSI WA UCHAPAJI,UUZAJI NA USAMBAZAJI VITABU NCHINI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akielezea lengo la Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa  Idara ya usimamizi wa Elimu Sekisheni ya Elimu ya awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambaye amemwakilishi Katibu Mkuu TAMISEMI Bi.Susana Nussu,akitoa neno wakati wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau  Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Kamishna wa Elimu nchini Dkt.Lyabwene Mtahabwa,akizungumzia dhamira ya mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wachapishaji Vitabu Tanzania, (PATA )Bw.Gabriel Kitu wakati akiwasilisha maoni na mapendekezo wakati wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wauza Vitabu Tanzania (BSAT) Bw.Albert Mwaipyana akiwasilisha maoni na mapendekezo wakati wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Uthibiti ubora wa shule kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Euphrasia Buchuma,akifafanua jambo kwa washiriki wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Morale Foundation for Education and Training (MOFET) Bw.Moses Kyando akichangia mada wakati wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Mhadhiri Msaidizi na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Chuo cha Biashara Godfrey Bukagile,akitoa maoni yake wakati wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, akijibu hoja mbalimbali wakati wa Mkutano wa Wadau Binafsi wa Uchapaji,Uuzaji na Usambazaji wa Vitabu nchini kikao kilichofanyika leo March 12,2022 jijini Dodoma.

 

………………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Prof. Adolf Mkenda, amefanya mkutano na wadau wa uchapishaji, usambazaji na uandishi wa vitabu vya shule ili kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa changamoto ya upungufu wa vitabu na kuongeza utamaduni wa usomaji.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma, Prof. Mkenda amewataka wadau hao kujadili kwa uwazi na ukweli juu ya changamoto zilizopo ili ziweze kutatuliwa na kuwezesha upatikanaji wa vitabu vyenye ubora, kwa wakati na bei nafuu hasa vya shule.

Prof.Ndalichako amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inawezesha shughuli za vitabu kwenda vizuri ili kuongeza idadi ya vitabu shuleni na kukuza usambazaji na usomaji wa vitabu kwa kuwa ubora wa elimu unakwenda sambamba na upatikanaji wa vitabu bora.

“Serikali inataka kuona Watanzania wengi zaidi wakiandika vitabu na kuvisambaza kama ilivyokuwa zamani ambapo watu walikuwa wanasoma zaidi lakini siku hizi imekuwa kinyume kabisa, tunataka utamaduni huo urudi sasa,” amesisitiza Prof. Mkenda.

 Prof. Mkenda amesema Serikali ilielekeza kuwa na kitabu kimoja cha Kiada kwa kila somo kinachotumika nchini kilichoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na kuruhusu matumizi ya vitabu vingine vya ziada vinavyoandaliwa na wachapishaji binafsi na kupata ithibati kutoka mamlaka husika.

Waziri Mkenda amesema Serikali haiwezi kufunga milango ya vitabu vingine vyenye ithibati kutumika shuleni kama vitabu vya ziada, hivyo ameagiza maafisa wote ambao wamekuwa wakizuia matumizi ya vitabu vyenye ithibati kutoka kwa waandishi binafsi kuacha mara moja na kwamba ambaye atapatikana akizuia vitabu hivyo atachukuliwa hatua.

Aidha ameagiza orodha ya vitabu vilivyopitishwa na mamlaka kutumika kama vya ziada visambazwe ili kuwezesha wazazi na walezi kuchagua na kuwanunulia watoto wao.

“Nasisitiza kuwa wazazi wapewe taarifa ya vitabu vya ziada vyenye ithibati ili waamue wenyewe lakini si kuwalazimisha kununua aina moja ya vitabu. Ni muhimu kuhimiza vitabu vingi zaidi kutumika ili kuwezesha watu kujua mambo mengi zaidi,” ameongeza Prof. Mkenda.

Hata hivyo Prof.Mkenda amemuagiza Kamishna wa elimu nchini Dkt.Lyabwene Mtahabwa,kuunda timu ndogo itakayoshirikisha Chama cha Wachapishaji nchini(PATA) na Chama cha Wauza Vitabu Tanzania (BSAT) ili kutatua kero za upatikanaji wa vitabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amesema wao kama mamlaka ya utoaji ithibati ya vitabu vya ziada wamezipokea changamoto zote zilizotolewa na wadau hao na kwamba watazifanyia kazi ili kuwezesha upatikanaji wa vitabu shuleni kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wachapishaji Vitabu Tanzania, Gabriel Kitu amemshukuru Waziri kwa kufanya mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa elimu nchini na kwa kuwapa nafasi ya kutoa changamoto wanazokutana nazo katika mchakato wa uandishi wa vitabu.

Kitu amesema changamoto kubwa inayojitokeza kwa upande wao ni kwa baadhi ya shule kuogopa kutumia vitabu vya wachapishaji binafsi vyenye ithibati, hivyo ameiomba Wizara kutoa maelekezo ya kuruhusu walimu kutumia vitabu hivyo kwa wanafunzi.

About the author

mzalendoeditor