Familia ya mtoto mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa wa Kitongoji cha Afya mji mdogo Katoro, imeiomba Serikali na wadau mbalimbali kuingilia kati ili mtoto wao aweze kupata haki yake baada ya kujeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri na mtuhumiwa Salome Joseph ambaye ameachiwa huru na Mahakama ya Mwanzo ya Katoro.
Mtoto huyo amejeruhiwa Februari 26, mwaka huu kwa kukatwa sehemu za siri baada ya kutuhumiwa kuiba shilingi 5,200 kwenye Duka la Sofia Salome mkazi Kitongoji cha Ibondo Mamlaka ya mji Mdogo wa Katoro.
CHANZO:GLOBAL TV