Featured Kitaifa

MBUNGE IKUPA AMSAIDIA MTOTO MWENYE MLEMAVU KITIMWENDO 

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa akiwasili katika Taasisi ya Al Mahdi Foundation eneo la Chinangali Jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa msaada wa kitimwendo (Wheelchair) kwa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil.

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa,akipata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Al MahdI Foundation,Mussa Palasa katika eneo la Chinangali Jijini Dodoma alipoenda kutoa msaada wa kitimwendo (Wheelchair) kwa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil.

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa,akimueleza jambo Mkurugenzi wa Taasisi ya Al MahdI Foundation,Mussa Palasa mara baada ya kwenda kutoa msaada wa kitimwendo (Wheelchair) kwa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil katika eneo la Chinangali Jijini Dodoma.

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa,akizungumza wakati akikabidhi  msaada wa kitimwendo (Wheelchair) kwa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil katika Taasisi ya Al Mahdi Foundation eneo la Chinangali Jijini Dodoma .

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa akikabidhi msaada wa kitimwendo (Wheelchair) kwa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil katika Taasisi ya Al Mahdi Foundation eneo la Chinangali Jijini Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa akiteta jambo na mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil mara baada ya kumsaidia kitimwendo (Wheelchair) katika Taasisi ya Al Mahdi Foundation eneo la Chinangali Jijini Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa akimkabidhi pesa kiasi cha shilingi laki moja Mama Mzazi wa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil mara baada ya kumsaidia kitimwendo (Wheelchair) katika Taasisi ya Al Mahdi Foundation eneo la Chinangali Jijini Dodoma

…………………………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

MBUNGE wa Viti Maalum kundi la walemavu (CCM) Mhe.Stella Ikupa ametoa kitimwendo (Wheelchair) kwa mtoto mwenye ulemavu,Feisal Fadhil ambacho kitamsaidia kwenda shule huku akiwataka wadau kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum.

Akizungumza  katika Taasisi ya Al Mahdi Foundation eneo la Chinangali Jijini Dodoma Mhe.Ikupa, amesema baada ya kupata taarifa juu ya mtoto huyo aliamua kumsaidia ili aweze kwenda shule.

“Tulikuwa katika eneo la Chinangali ambapo nimeweza kumpatia mtoto mwenye ulemavu kitimwendo  baada ya kupata taarifa.Ninamshukuru Mungu kuweza kumkabidhi hivi viti changamoto ni anapelekwa katika shule gani?

“Kwa sababu amefikisha umri wa kwenda shule kwa sababu mama yake mzazi hawezi kumbeba kwa sababu mtoto ni mkubwa hawezi kumbeba na anawatoto mapacha yaani mtoto mwenye ulemavu ana pacha wake inakuwa ngumu kumbeba yule pacha ameishaanza shule lakini huyu mwingine bado kwa sababu mama yake anashindwa kumbeba,”amesema.

Pia, amesema amemsaidia kiasi cha shilingi laki moja mama mzazi wa mtoto huyo ili aweze kujiajiri pamoja na kufanya shughuli ndogondogo.

“Nimepa huyu mama hela kidogo ili aweze kufanya kitu chochote ili aweze kufanya biashara yoyote.Hata mtu anauza mayai anaongeza kipato naamini mama huyu hii hela itamsaidia kufanya biashara.

“Mimi nikiwa kama Mbunge wa chama cha Mapiunduiz Rais Samia aliweza kukutana na watoto wenye ulemavu naendelea kufuata nyendo za Rais Mama yetu anatupenda Kama watanzania hatuna kitu cha kumlipa zaidi ya kuendelea kumshukuru kumupmbea kwa Mungu”amesema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya Al MahdI Foundation,Mussa Palasa ambayo inafanya kazi ya kusaidia jamii isiyojiweza wakiwemo Yatima,wajane,wazee ,Vijana na walemavu amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa kutoa msaada huo.

“Kwa  niaba ya mtoto wetu Feisal Fadhil ambaye leo ameweza kukabidhiwa Taasisi inatoa shukrani kubwa kwa Mheshimiwa, Mwenyezimungu amemjaalia kumpa moyo wa kuweza kutufikishia hichi, Mwenyezimungu ambariki sana na tunawaomba wadau  wengine  kutusaidia,”amesema.

Naye mzazi wa  mtoto, Magreth Mlalikwa amesema anamshukuru Mbunge Ikupa  kwa kumsaidia mtoto wangu hiki kitimwendo kitamsaidia katika kwenda Shule hivyo nawaomba  wadau wengine kuiga mfano huo.

“Namshukuru   Mungu kwa kumsaidia mtoto wangu na nashauri watu wengine wajitokeze kumsaidia kama hawa walemavu namshukuru sana Mbunge Ikupa sina cha kumlipa kwa moyo wake wa kusaidia wengine zaidi namuombea kwa Mungu azidi kumlinda na kumbariki kila siku ,”amesema

About the author

mzalendoeditor