Featured Michezo

PITSO MOSIMANE AONGEZA MKATABA MPYA NDANI YA AL AHLY SC

Written by mzalendoeditor

Kocha Mkuu wa klabu ya Al Ahly SC ya Misri, Pitso Mosimane (57) raia wa Afrika Kusini ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi msimu wa 2023/24.

Mosimane alitangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Oktoba mwaka 2020 akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Ameiongoza timu hiyo katika michezo 83 akipata ushindi katika michezo 59 akipoteza michezo 7 na kutoka sare michezo 17 huku akitwaa makombe matano na kuchukua medali za Kombe la Dunia la FIFA mara mbili.

About the author

mzalendoeditor