RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Machi 8, 2022 amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi kwa kuigawa iliyokuwa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto kuwa Wizara mbili na kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 8, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A. Said.
Aidha Mhe. Rais pia amewateua Mawaziri wapya wanne na Naibu Mawaziri wapya saba. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:
1. OFISI YA RAIS
i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu
Mhe. Jamal Kassim Ali. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jamal alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.
ii. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed (hajabadilishiwa Wizara)
iii. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora  Mhe. Haroun Ali Suleiman (hajabadilishiwa Wizara)
iv. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga (hajabadilishiwa Wizara)
v. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Saada alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
2. OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harusi Said Suleiman
3. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe. Hamza Hassan Juma
4. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Khalid alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi.
5. Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis
6. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Mhe. Lela Muhamed Mussa. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Lela alikuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
7. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita (hajabadilishiwa Wizara)
8. Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
Mhe. Rahma Kassim Ali. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Rahma alikuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.
9. Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaib Hassan Kaduara
10. Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Suleiman alikuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini.
11. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Simai Mohamed Said. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simai alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
12. Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui. Kabla ya uteuzi huo Mhe. Nassor alikuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto (hajabadilishiwa Wizara)
13. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma. Kabla ya hapo Mhe. Riziki alikuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.
14. Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban (hajabadilishiwa Wizara)
NAIBU MAWAZIRI:
1. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Ali Suleiman Ameir (Mrembo)
2. Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Juma Makungu Juma
3. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Abdulgullam Hussein
4. Naibu Waziri, Wizara ya Afya Mhe. Hassan Khamis Hafidh
5. Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Anna Athanas Paul
6. Naibu Waziri, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaaban Ali Othman
7. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe. Nadir Abdullatif Yussuf Alwardy
Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 08 Machi, 2022.
Mawaziri wapya na wale waliobadilishiwa Wizara, pamoja na Naibu Mawaziri wataapishwa siku ya Alkhamis tarehe 10 Machi, 2022 saa 3.00 asubuhi Ikulu Zanzibar.
Previous articleTBA YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Next articleWIZARA YA HABARI,MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here