Featured Michezo

SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI,COASTAL UNION YANG’ARA UGENINI

Written by mzalendoeditor
Na Alex Sonna-DODOMA
KLABU ya Simba imeendelea kutoa dozi ya uhakika kwa kwenye ligi ya NBC mara baada ya kuizamisha mabao 2-0 Dodoma jiji kutoka makao makuu ya nchi mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko zikiwa ngoma mbichi ya bila kufungana.Simba walirudi kipindi cha pili kwa nguvu na mashambulizi makali katika lango la Dodoma jiji na mnamo dakika ya 55 Clautos Chama alifunga bao kwa mkwanju wa penalti baada ya beki wa Dodoma kuunawa moira ndani ya 18 na mwamuzi kuamua kuweka tuta.
Simba walipata bao la Pili dakika ya 75 likifungwa na Meddie Kagere na kuamsha shangwe kwa mashabiki walifika katika mchezo huo.Kwa ushindi huo Simba wamefikisha pointi 37 nafasi ya pili wakizidiwa Pointi 8 na Vinara Yanga wenye Pointi 45 huku Dodoma Jiji wakibaki nafasi ya kumi na moja wakiwa na Pointi 18.
Mechi nyingine Ruvu Shooting wameshindwa kung’ara katika uwanja wao baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Biashara United huku Chamazi Complex wenyeji KMC wamechapwa mabao 3-2 na Coastal Union.
 

About the author

mzalendoeditor