Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI BENJAMINI MKAPA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa Emanuel Mzena mara baada ya kuwasili Shuleni hapo leo tarehe 07 Machi, 2022 kwa ajili ya kuzungumza na Wanafunzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Emanuel Mzena mara baada ya kuwasili Shuleni hapo leo tarehe 07 Machi, 2022 kwa ajili ya kuzungumza na Wanafunzi wa Shule hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akigawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Shule ya Msingi Uhuru pamoja na Shule ya Uhuru Mchanganyiko leo tarehe 07 Machi, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Wanafunzi wa Shule ya uhuru Mchanganyiko na Uhuru Msingi zilizopo eneo la Gerezani Ilala Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Machi, 2022.

……………………………………………….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inafanya jitihada ya kuweka mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia ili kila Mtanzania anufaike na fursa za elimu kwa manufaa yake binafsi na taifa kwa ujumla.

Rais Samia amesema hayo wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo, iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Samia pia amesema Serikali imeendelea na Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/2022 hadi 2025/ 2026 ambao utazingatia utoaji elimu jumuishi katika ngazi zote za elimu ili kuwanufaisha pia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Pamoja na kujenga shule na madarasa ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na jumuishi, Serikali  imeshatumia zaidi ya shilingi bilioni 5.9 kununua vifaa kwa ajili ya wanafunzi hao katika elimu ya msingi, sekondari na vyuo. 

Mbali na hapo, Serikali imetoa mafunzo ya aina tofauti kwa walimu 3980 wenye taaluma ya Elimu Maalum katika ngazi ya Msingi, Sekondari na Ualimu.

Mafunzo hayo yametolewa kwa wadhibiti ubora ili waweze kukagua madarasa maalum na jumuishi pamoja na miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. 

Wakati huo huo, Serikali ilifanya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ambao wamefikisha umri wa kuanza shule na kubaini watoto 28,698 wenye mahitaji maalum kati ya 59,784 waliochunguzwa. 

Ili kuhakikisha watoto wote wenye mahitaji maalum wanapata fursa ya elimu tayari watoto hao wote wameshaandikishwa shule.

About the author

mzalendoeditor