Wydad Casablanca ya Morocco, wamemshtaki Mchezaji Mtanzania Simon Msuva kwa Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kuwa amevunja mkataba bila sababu.

Hata hivyo, Msuva naye amewashtaki Wydad kwa FIFA pia kuwa hajalipwa pesa zake muda mrefu na miamba hiyo ya Afrika.

Kesi hizo zimemuweka njia panda Msuva ambaye alikuwa anakaribia kumalizana na timu moja huko Uturuki ambapo sasa atasubiri kesi hizo FIFA zimalizike kujua hatma yake.

Msuva bado amesalia nchini akigoma kuendelea kuichezea klabu hiyo kutokana na kutomlipa fedha zake kwa muda mrefu.

Previous articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MARCH 6,2022
Next articleMAYELE AZIDI KUTETEMA ,YANGA YAICHAPA GEITA GOLD FC CCM KIRUMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here