Featured Michezo

WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO YAMSHTAKI FIFA SIMON MSUVA

Written by mzalendoeditor

Wydad Casablanca ya Morocco, wamemshtaki Mchezaji Mtanzania Simon Msuva kwa Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kuwa amevunja mkataba bila sababu.

Hata hivyo, Msuva naye amewashtaki Wydad kwa FIFA pia kuwa hajalipwa pesa zake muda mrefu na miamba hiyo ya Afrika.

Kesi hizo zimemuweka njia panda Msuva ambaye alikuwa anakaribia kumalizana na timu moja huko Uturuki ambapo sasa atasubiri kesi hizo FIFA zimalizike kujua hatma yake.

Msuva bado amesalia nchini akigoma kuendelea kuichezea klabu hiyo kutokana na kutomlipa fedha zake kwa muda mrefu.

About the author

mzalendoeditor