Featured Kitaifa

WATUMISHI DAWASA WATAKIWA KUBORESHA UFANISI

Written by mzalendoeditor

WATUMISHI wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wametakiwa kuthamini kazi ya kutoa huduma ya Majisafi na usafi wa Mazingira kwa wateja na kuitenda kwa ufanisi mkubwa.

Akiongea katika kikao kazi cha wafanyakazi wote kilichofanyika hivi karibuni, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema huduma ya maji ni huduma takatifu hivyo kila mtumishi anapaswa kufanya wajibu wake kwa uaminifu mkubwa.

“Sote tunapaswa kuelewa kwamba kufanya kazi katika Sekta ya maji ni kwa kusudi maalum na sio kwa bahati mbaya, hivyo kila mtumishi ana mchango sahihi katika kukuza maendeleo ya Mamlaka” alisema Mhandisi Luhemeja.

Aliongeza kuwa kila mtumishi wa mamlaka analo jukumu la kutengeneza mazingira mazuri ya kuishi kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kupitia huduma ya majisafi kwa  kuhakikisha upotevu wa maji unadhibitiwa ili kuboresha upatikanaji wa maji kwa wateja.

About the author

mzalendoeditor