Featured Kitaifa

TRA TANGA WAIKABIDHI WILAYA YA BUHIGWE PIKIPIKI MBILI KWA AJILI YA KUWASAIDIA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA KITAIFA

Written by mzalendoeditor

KAIMU
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga  Davis Mongate
kushoto akimkabidhi pilikipiki mbili Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali
Kanali Michael Ngayalina kwa ajili ya kuwasaidia kutekeleza majukumu ya
Kitaifa leo Jijini Tanga
Mkuu
wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina kulia akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo leo  kushoto ni KAIMU Meneja wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga  Davis Mongate

Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali Michael Ngayalina akikagua pikipiki
mbili ambazo wamekabidhiwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Kamishna
wa Forodha kwa ajili ya kuwasaidia kutekeleza majukumu ya Kitaifa leo
Jijini Tanga

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga leo wameikabidhi wilaya ya
Buhigwe ya Mkoani Kigoma pikipiki mbili kwa ajili ya kuwasaidia katika
majukumu mengine ya kitaifa

Pikipiki hizo zilikamatwa na maofisa
wa TRA kwa nyakati tofauti wakati wakifanya doria ambazo zilikutwa
zikiwa vimebeba biashara ya magendo huku watuhumiwa wakikimbia

Halfa
ya makabidhiano hayo imefanyika leo mkoani Tanga ambapo Kwa niaba ya
Meneja wa Mkoa wa Tanga Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga na Kamishna wa
Forodha, Davis Mongate .

Alisema leo ni siku ramsi ya
kuzikabidhi kwa Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali Michael
Ngayalina ili ziweze kuwasaidia majukumu mengine ya kitaifa ambazo
zilikamatwa wilaya Pangani zikiwa zimepakia madumu ya mafuta ya magendo.

Aidha alisema maafisa hao walizikamata na wahusika walikimbia
na kuzitekeleza pikipiki hizo na Kamisha wa forodha alizigawa kwa Mkuu
wa wilaya ya Buhigwe ambapo huo ni utaratibu wa mamlaka vitu ambavyo
vinakamatwa kinyume cha utaratibu zinagawiwa kwenye taasisi za serikali .

Akizungumza mara baada ya kupokea pikipiki hizo, Kanali Michael
alimshukuru Kamisha wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA
Tanzania na Wizara ya Fedha kwa niaba ya wananchi wake kwa kuwapatia
vyombo hivyo vya usafiri ambazo zilikamatwa zikifanya shughuli za
magendo.

Alisema wilaya yao bado inachangmoto nyingi za
kiusalama lakini kibiashara ni wilaya ya mpakani hivyo pikipiki hizo
zitawasaidia shughuli za doria na biashara mpakani na biashara
inayokinzana na sheria, kanuni za serikali hususani idara ya mapato
pikipiki hizo zitawasaidia.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi
ni vizuri wakafuata sheria ,taratibu na kanuni kwenye ufanyaji biashara
kwani wizara ya fedha imeeleza wananachi kutoa kodi mbalimbali na
kufuata utaratibu uliotolewa na serikali kufanya biashara na kuepuka na
vitendo vinavyokinzana na sheria hususani magendo.

“Hapa
nimeambiwa wamiliki wa pikipiki hizi walikimbia baada ya kukamatwa na
maafisa wa idara ya forodha tunaomba wananchi fuateni sheria na kanuni
tufanye biashara na kupekna na kukidhana na vyombo hivyo “Alisema

“Tumekuja
kuvifuata baada ya kupokea taarifa kwamba tumegawiwa hivyo tutakwenda
kuvitumia kwa shughuli za kibiashara na kiusalama kwani wilaya ina
takribani kilomita 60 za mpaka na Burundi na changamoto za kiusalama na
biashara ni kubwa tunahaidi vyombo hivi vitatumika kwa shughuli hizo na
sio nyenginevyo”Alisema

Awali akizungumza kwa niaba ya Meneja wa
Mkoa wa Tanga Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga na Kamishna wa Forodha,
Davis Mongate alisema leo wamemua kuzigawa pikipiki kwa Mkuu wa wilaya
ya Buhigwe Mkoani Kigoma kwa ajili ya kusaidia majukumu ya Kitaifa
ambapo zilikamatwa wilaya ya Pangani zikiwa zimepakia madumu ya mafuta
na wenye pikipiki walikimbia.

Alisema huo ni utaratibu wa
mamlaka kwamba vitu ambavyo vinakamatwa kinyume na taratibu vinagawiwa
kwa Taasisi za Serikali zenye upungufu wa vyombo vya usafiri kwa hizo
pilipiki zitakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Buhigwe .

About the author

mzalendoeditor